SZone


Pages

Wednesday, April 4, 2012

Wanaume wengi wagumba Tanzania


Utafiti Nchini Tanzania Wabaini


“17% hawana kabisa mbegu zenye uwezo wa kutungisha mimba, zaidi ya maji tu.”

Kubeba ‘Laptop’ balaaa! unene sana tatizo na kazi jeshini nomaa!!

  • Maprofesa Chuo Kikuu Muhimbili Watoa Sababu Za Kuongezeka Kwa Tatizo.

UTAFITI mpya umebaini kuwa nusu ya wanaume nchini Tanzania ni wagumba. Kwa mujibu wa utafiti huo, uliofanywa na Chuo kikuu cha Tiba Muhimbili kati ya 2009 na Septemba 2010, ni 47.05% ya wanaume wanaokwenda kupima afya zao za uzazi, hawana uwezo wa kutungisha mimba, kati ya wanaume 221 waliopimwa, ni 30.03% walikuwa na mbegu dhaifu na 17.02% walikuwa hawana kabisa mbegu zenye uwezo wa kutungisha mimba, zaidi ya maji tu.

Sababu za ugumba
Bongo Live® imebaini sababu za ugumba kwa mwanaume kuwa ni uambukizo katika tezi inayozalisha manii (shahawa), sababu nyingine za ugumba kwa wanaume ni kemikali zinazoingia katika miili yao, mionzi na wakati mwingine ajali inapoathiri tezi hiyo.

Walio hatarini sana kuwa wagumba
Wanaoathirika zaidi ni wale wanaofanya kazi migodini, jeshini au wanaozungukwa na kemikali kwa muda murefu.

Sababu nyingine ni joto kuzidi katika sehemu za siri za mwanaume, kubeba laptop, unene kupita kiasi na mazingira.

Shahawa zipi salama
Kutokana na tafiti za kisayansi na kipimo cha kitaalamu cha manii ‘shahawa’ kama zipo salama, rangi ya mbegu pamoja na umbile huangaliwa ilikutambua ubora wake. Hata kwa kuziangalia tu, “mbegu zenye rangi ya kijivu au nyeupe si salama”

Migogoro ya kifamilia
Mara nyingi tatizo liko kwa mwanaume, lakini kuna tabu ya kuwaeleza ukweli, wengi hawataki kukubali, jambo kama hilo huleta migogoro ya kifamilia, kwani huenda mwanamke amekwisha mzalia mumewe watoto ambao kimantiki si wa kwake.

Bongo Live® inataadharisha, “Pengine mwanaume aliwai kupata watoto hapo awali, lakini sasa hivi hapati, bado atakuwa mgumba, na wanawake wagumba wapo, ni vyema kwenda kupima afya ya uzazi kwa wana ndoa kama ilivyokuwa kwa kupima VVU/UKIMWI”

Aina za ugumba
Bongo Live® imebaini kuna ugumba wa aina mbili; wa kuzaliwa nao na ugumba unaopatikana ukubwani, wapo wanaozaliwa na ugumba, yaani mbegu zao ama ni dhaifu au hawana kabisa mbegu tangu kuzaliwa kwao.

Ujazo wa shahawa kuweza kutungisha mimba
Bongo Live® imebaini kuwa, ujazo wa manii (shahawa) anaopaswa kuwa nao mwanaume ili aweze kutungisha mimba ni miligramu moja na nusu hadi nne na nusu. Ujazo wa manii ukipungua au ukizidi, basi mbegu hizo zina matatizo.

Mwanaume mmoja kati ya saba wanaokwenda kupima afya ya uzazi hugundulika na matatizo ya ugumba. (www.who.org/utafiti2009duniani)

3 comments: