SZone


Pages

Monday, October 22, 2012

Jinsi ya Kudumu na Mpenzi wako





Jamaa na Kimada wake watembezwa mitaani baada ya kufumaniwa, hii ni kwa sababu ya kutolidhishwa na wapenzi wao.

Epukana na AIBU kama hii, mlidhishe mwenzio

Je, Wataka Kudumu na Mpenzi Wako?

Jaribu kufuata mambo NANE [8] yafuatayo:-


  1. Kila unaporudi nyumbani kutoka safari, kazini ama katika shughuli zako, jitahidi kumchukulia zawadi hata kama ni pipi!
  2. Pendelea sana kumtania kimahaba mpenzi wako.




  3. Epuka kununa nuna hovyo ukiwa na mpenzi wako... ugomvi hachana nao







4. Jijengee tabia ya kumsifu mpenzi wako wakati wowote
5. Pendelea kutambua matatizo yake [si lazima uwe na HELA, PESA ama FEDHA]
6. Usipendelee kumkumbusha ya zamani haswa yanayomchukiza
7. Fikiria mema yake kabla ya kuhesabu mabaya yake
8. Mliwaze anapokasirika, msaidie kwa kila jambo lililondani ya uwezo wako

Utafiti uliofanywa waonyesha kuwa mjali mpenzi wako kwa kila jambo kwani mpenzi ni mpenzi na mapenzi hayana umri, uzoefu, pesa, hela, fedha, kabila au dini.
 Hawa ni baadhi ya wapenzi walio ahidiana kupenda mpaka mmoja wao kufa........ Wewe je?

Tabia ya kufuatana fuatana mpaka sehemu za kazi, vijiweni ama na kwingineko na kukwidana nguo haifai








Sunday, July 29, 2012

Wanawake waongoza kuvaa chupi zilizotoboka

Utafiti Tanzania Wabaini

WANAWAKE WENGI WANAVAA CHUPI ZILIZOTOBOKA


“85% hawavai kabisa chupi za rangi nyeupe” Sasa hawavai gagulo

·         Wanafunzi wa vyuo Watoa Sababu Za Kuongezeka Kwa Tatizo.




UTAFITI mpya umebaini kuwa nusu ya wanawake nchini Tanzania uvaa chupi zilizotoboka ama kuchanika. Kwa mujibu wa utafiti huo, uliofanywa na Bongo-Live kwa wanafunzi wa Vyuo mbalimbali nchini Tanzania. Kati ya wasichana 10 ni wawili tu uvaa chupi nyeupe, ni 85% ya wanawake hawavai kabisa chupi ya rangi nyeupe.

Sababu za kutovaa chupi nyeupe
Bongo Live® imebaini sababu za kutovaa chupi nyeupe kwa mwanawake hao kuwa ni kutokuwa wasafi na kushindwa kuzitunza kwa rangi yake. Wanafunzi hao inasemekana kuwa wanaelemewa na masomo kiasi cha kushindwa kupata muda wa kufua hata waendapo kuoga.


Sababu za kutoboka kwa chupi
Bongo-Live, Imebaini kuwa wanawake wengi wanachupi nyingi na pamoja na wingi wa chupi walizonazo bado uvaa zilizotoboka ama zilizochanika. Hii inatokana na hali halisi ya kuvua pindi waendapo haja ndogo, chupi uzivua mpaka usawa wa mapaja kwa kitendo cha kuchuchumaa uvuta chupi na kufanya nyuzi kulegea ama kutatuka kwa chupi. Pia imeelezwa kwamba, uvaaji, ufuaji na kuanikwa kwa vazi hilo chini ya godoro mara kwa mara usababisha tatizo hilo.
Sababu nyingine ni joto kuzidi katika sehemu za siri za mwanamke, unene kupita kiasi na mazingira yanayowazunguka.

Wednesday, April 4, 2012

Wanaume wengi wagumba Tanzania


Utafiti Nchini Tanzania Wabaini


“17% hawana kabisa mbegu zenye uwezo wa kutungisha mimba, zaidi ya maji tu.”

Kubeba ‘Laptop’ balaaa! unene sana tatizo na kazi jeshini nomaa!!

  • Maprofesa Chuo Kikuu Muhimbili Watoa Sababu Za Kuongezeka Kwa Tatizo.

UTAFITI mpya umebaini kuwa nusu ya wanaume nchini Tanzania ni wagumba. Kwa mujibu wa utafiti huo, uliofanywa na Chuo kikuu cha Tiba Muhimbili kati ya 2009 na Septemba 2010, ni 47.05% ya wanaume wanaokwenda kupima afya zao za uzazi, hawana uwezo wa kutungisha mimba, kati ya wanaume 221 waliopimwa, ni 30.03% walikuwa na mbegu dhaifu na 17.02% walikuwa hawana kabisa mbegu zenye uwezo wa kutungisha mimba, zaidi ya maji tu.

Sababu za ugumba
Bongo Live® imebaini sababu za ugumba kwa mwanaume kuwa ni uambukizo katika tezi inayozalisha manii (shahawa), sababu nyingine za ugumba kwa wanaume ni kemikali zinazoingia katika miili yao, mionzi na wakati mwingine ajali inapoathiri tezi hiyo.

Walio hatarini sana kuwa wagumba
Wanaoathirika zaidi ni wale wanaofanya kazi migodini, jeshini au wanaozungukwa na kemikali kwa muda murefu.

Sababu nyingine ni joto kuzidi katika sehemu za siri za mwanaume, kubeba laptop, unene kupita kiasi na mazingira.

Shahawa zipi salama
Kutokana na tafiti za kisayansi na kipimo cha kitaalamu cha manii ‘shahawa’ kama zipo salama, rangi ya mbegu pamoja na umbile huangaliwa ilikutambua ubora wake. Hata kwa kuziangalia tu, “mbegu zenye rangi ya kijivu au nyeupe si salama”

Migogoro ya kifamilia
Mara nyingi tatizo liko kwa mwanaume, lakini kuna tabu ya kuwaeleza ukweli, wengi hawataki kukubali, jambo kama hilo huleta migogoro ya kifamilia, kwani huenda mwanamke amekwisha mzalia mumewe watoto ambao kimantiki si wa kwake.

Bongo Live® inataadharisha, “Pengine mwanaume aliwai kupata watoto hapo awali, lakini sasa hivi hapati, bado atakuwa mgumba, na wanawake wagumba wapo, ni vyema kwenda kupima afya ya uzazi kwa wana ndoa kama ilivyokuwa kwa kupima VVU/UKIMWI”

Aina za ugumba
Bongo Live® imebaini kuna ugumba wa aina mbili; wa kuzaliwa nao na ugumba unaopatikana ukubwani, wapo wanaozaliwa na ugumba, yaani mbegu zao ama ni dhaifu au hawana kabisa mbegu tangu kuzaliwa kwao.

Ujazo wa shahawa kuweza kutungisha mimba
Bongo Live® imebaini kuwa, ujazo wa manii (shahawa) anaopaswa kuwa nao mwanaume ili aweze kutungisha mimba ni miligramu moja na nusu hadi nne na nusu. Ujazo wa manii ukipungua au ukizidi, basi mbegu hizo zina matatizo.

Mwanaume mmoja kati ya saba wanaokwenda kupima afya ya uzazi hugundulika na matatizo ya ugumba. (www.who.org/utafiti2009duniani)